Na Ramadhan Hassan,Dodoma
WAKALA wa Vipimo(WMA) umewataka watanzania pindi wanapoagiza mchanga ama kokoto kwa ajili ya ujenzi kuagiza kwa mita za ujazo na sio kwa tripu ya gari.
Hayo yameelezwa leo Machi 25,2025 na Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa WMA katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita.
“Wanaonunua mchanga ama kokoto wasinunue kwa kuagiza gari bali waseme wanaagiza kwa mita za ujazo na huwa ujazo huo umeandikwa pembeni ya gari unapoagiza agiza kwa mita za ujazo,”amesema Mtendaji huyo wa WMA.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema anaotumia mizani kuacha dhuluma na kupunja kwani hata vitabu vya dini vinazungumzia haki kwenye vipimo.
Kihulla amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mizani isiyo sahihi wengine wakipunguza mawe ya mizani ili kupata faida na kuwapunja wateja.
Pia amesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Wakala ilipanga kuhakiki vipimo Milioni 3,923,652 vitumikavyo katika sekta mbalimbali.

Amesema Wakala umefanikiwa kuhakiki vipimo 3,668,149 sawa na Asalimia 94 ya Malengo.
Hata hivyo Afisa huyo amesema ili kutimiza azima ya kumlinda mlaji Wakala imepewa dhamana ya kusimamia Kisheria matumizi sahihi ya vipimo Kwa kutekeleza majukumu ya kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika kwenye sekta mbalimbali.
Crédito: Link de origem