Na Nora Damian, Mtanzania Digital
Benki ya CRDB imetenga zawadi za fedha taslimu, magari na simu janja kwa wateja wake ambazo zitatolewa kupitia kampeni mpya ya SimBanking Humu Tu.
Akizungumza leo Machi 27,2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Kaimu Mkuu wa Biashara na Mkurugenzi mwenye dhamana ya uendeshaji matawi wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul, amesema lengo ni kuongeza hamasa kwa jamii juu ya matumizi ya Simbanking.
Amesema huduma bora za kisasa za benki hiyo zinaendana na matakwa ya wateja wao ambapo wamekuwa wakitumia fursa za kiteknolojia kubuni huduma mbalimbali.
“Simbanking ndio ‘Application’ ya kwanza kwenye soko letu, imeleta mapinduzi makubwa katika kuchochea huduma za kifedha Tanzania.
“Huduma za Simbanking zilianza mwaka 2011 na zimetoa fursa kwa Watanzania wengi kujiunga rasmi na mfumo wa kibenki ambao unapatikana kwa saa 24. Wateja zaidi ya milioni tatu wamejiunga na Simbanking na wanafanya miamala kwa kutumia Simbanking wakati wote,” amesema Paul.

Aidha amesema kupitia kampeni ya Benki ni Simbanking Humu Tu, zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wateja kama vile magari mapya, Tembo Points, Laptop
mpya na smartphones kwa wanafunzi wa vyuo.
“Zaidi ya Shilingi milioni 240 zitatolewa kila baada ya miezi miwili, kutakuwa na zawadi ya gari aina ya IST new model, Iphone 16 kila baada ya miezi mitatu kwa wanafunzi wa vyuo na hadi Desemba tutakapofikia mwisho wa kampeni tutakuwa tumempata mshindi wa jumla ambaye atazawadiwa Toyota Harrier New Model,” amesema Paul.
Amewahimiza wateja wa benki hiyo kufanya miamala kupitia Applikesheni ya Simbanking au kwa kubonyeza 15003#.
Nao mabalozi wa Benki ya CRDB, Mwanamuziki Rayvan, Hamisa Mobeto na Aziz Ki, wameipongeza benki hiyo kwa kuzindua kampeni hiyo na kuwahamasisha Watanzania ambao hawana akaunti kwenda kufungua na kuunganishwa na Simbanking ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali.
Crédito: Link de origem