top-news-1350×250-leaderboard-1

Watanzania jiepusheni n watu wenye nia ya kuvunja amani-Sheikh Rajabu

Na Ramadhan Hassani, Mtanzania Digital

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu, amewataka Watanzania kuendelea kulinda amani ya nchi na kuepuka vishawishi vya watu wenye nia mbaya kwa taifa. Akizungumza leo, Jumatatu Machi 31, 2025, katika swala ya Eid El Fitri iliyofanyika katika Msikiti wa Gaddafi jijini Dodoma, Sheikh Rajabu alisisitiza kuwa maendeleo yanapatikana kutokana na kuwepo kwa amani, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuilinda kwa nguvu zote.

“Ikiondoka tunu ya amani hatuwezi kukaa. Tumeona mifano jinsi amani ilivyopotea Palestina na Kongo. Ndugu zangu, hatuna budi kuliombea taifa letu na kumuombea Mama Samia ili aendelee kutuongoza vyema,” alisema Sheikh Rajabu.

Aliwataka Watanzania kutojihusisha na vishawishi vyovyote vinavyotokana na maslahi ya watu binafsi wasio na nia njema na nchi. Pia, aliwasihi waumini waendelee kutenda matendo mema hata baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na kutaja neema za Mwenyezi Mungu.

Watanzania jiepusheni n watu wenye nia ya kuvunja amani-Sheikh Rajabu

Katika hatua nyingine, Sheikh Abdulaziz Hilal aliwakumbusha waumini wa Kiislamu kuchunga mipaka ya sherehe baada ya kumaliza mwezi wa Ramadhani. Akizungumza katika uwanja wa Jamhuri, Sheikh Abdulaziz, ambaye ni Imamu wa Msikiti wa Bilal Area C, alisema waumini wanapaswa kutumia Iddi kwa kula na kunywa vya halali, huku wakiendelea kudumu katika ibada.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.