top-news-1350×250-leaderboard-1

Wadau wakutana kujadili rasimu ya maendeleo

Dar es Salaam. Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) limekutana na wadau mbalimbali ili kupokea maoni ya rasimu ya maendeleo ya viwanda yatakayowezesha kufikia malengo, shabaha na kutekeleza mikakati ya kuendeleza sekta ya viwanda nchini.

Baadhi ya maoni yaliyopokelewa  kwenye kikao hicho ni pamoja na masuala ya umeme, malighafi, teknolojia, kodi na rasilimali watu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Machi 11, 2025 katika huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Hashil Abdallah amesema rasimu hiyo imeandaliwa na kikundi kazi maalumu hivyo maoni yao yanakwenda kuweka mazingira wezeshi kwenye uzalishaji.

“Mkutano huu unatafsiri kwa vitendo dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuweka mazingira wezeshi kwenye uzalishaji viwandani na biashara,” amesema Dk Abdallah.

Dk Abdallah amewahakikishia wadau wote kuhusu maoni walioyatoa katika kufanya maboresho ya sera ya maendeleo ya viwanda wameyachukua na watayafanyia kazi,  kwa kuyachakata ili kuweka misingi ya uchumi.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dk. Hashil Abdallah akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi maalamu cha kikundi cha viwanda,jijini Dar es Salaam.Picha na Michael Matemanga

Naye, Katibu Mtendaji wa TNBC, Dk Godwill Lwanga amesema wamepokea maoni kutoka kwa wajumbe na wadau wa uchumi na sekta zote za biashara na wamekubaliana, ila  kwa wanaoendelea kutoa maoni wapeleke hadi Machi 18 mwaka huu.

“Katika kikundi kazi hiki tumekuwa na wawakilishi kutoka sekta zote katika kila nyanja na tunategemea sera hiyo pamoja na mkakati wake itazinduliwa kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha 2024/25 na kutumika kwa awamu ya uongozi utakaokuwepo,” amesema Dk Lwanga.

Amesema sera hiyo imejaribu kuangalia masuala yote ya teknolojia ya kidijitali kwa hiyo wanategemea kuwa viwanda vyote vitakavyokuja vitatumia teknolojia hiyo na haitaathiri mazingira.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni za AmiHamza, Amir Hamza amesema ushirikishwaji wa kutoa maoni utatengeneza mazingira rafiki ya uzalishaji, kwani wanatoa maoni kulingana na changamoto zilizopo.

Amesema maoni yanayokusanywa yasiishie kwenye viwanda vya Dar es Salaam bali yafike hadi mikoani hususan kwenye viwanda vilivyopo jirani na mipaka ya nchi, ili kujua changamoto zilizopo katika kuboresha sera za viwanda.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.