top-news-1350×250-leaderboard-1

Tuzo za Kariakoo Business Award ni mkakati wa kukuza uchumi

Na Mwandishi Wetu

Tuzo za Kariakoo Business Award zinatarajiwa kufanyika hivi karibuni katika Mkoa wa Dar es Salaam, zikiwa na lengo la kutambua na kuthamini mchango wa wafanyabiashara wa Kariakoo katika kukuza uchumi wa Taifa.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni katika uzinduzi wa tuzo hizo na Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa, ambapo amewahimiza wafanyabiashara kusajili biashara zao ili kuepuka migogoro ya umiliki.

“Ukisajili biashara yako, hata ukishinda tuzo, inakuwa mali yako halali. Lakini usiposajili, mtu mwingine anaweza kudai umiliki,” amesema Nyaisa, akitoa mfano wa mgogoro wa hivi karibuni kuhusu tamasha la Mtoko wa Pasaka, ambao tayari umemalizika.

Akizungumza mmoja wa waandaaji wa tuzo hizo, Frank Mbwana, akishirikiana na Zakayo Shushu, amesema lengo ni kuthamini juhudi za wafanyabiashara wa Kariakoo na kuwahamasisha kuendelea kukuza sekta hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka Watanzania kuwaunga mkono wafanyabiashara wa Kariakoo na kushirikiana nao kwa maendeleo ya biashara nchini.

“Tuzo hizi zimekuja wakati muafaka na katika eneo muhimu la biashara. Sikutarajia kuona muitikio mkubwa wa wafanyabiashara,” amesema Mpogolo.

Naye Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Kumbilamoto, amepongeza mshikamano wa wafanyabiashara wa Kariakoo na juhudi zao za kukuza uchumi wa jiji.

Kwa upande wake, Seveline, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, amesema kuanzishwa kwa tuzo hizi kutasaidia kuongeza ushindani wa kibiashara na kuimarisha ufanisi katika sekta hiyo.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.