top-news-1350×250-leaderboard-1

TANESCO yapata mbinu kuondoa tatizo la umeme kukatika SGR

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) limetaja sababu za kukatika kwa umeme katika treni ya mwendakosi (SGR) huku likidai lipo mbioni kuanzisha mkoa maalumu kwa ajili ya kushughulikia changamoto za umeme katika treni hiyo.

Hayo yameelezwa leo Machi 26,Jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Mhandisi Gissima Nyamohanga wakati akieleza mafanikio na mwelekeo wa Shirika hilo kuelekea miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Mpango wa Shirika ni SGR kuwa Mkoa ili kuweza kutatua changamoto na watakuwa na meneja uratibu ambaye atakuwa akishughulikia mradi huo pekee ambaye atakuwa na timu maalumu.

“Timu maalumu ambayo kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika,”amesema Mkurugenzi huyo.

Kuhusu kukatika kwa umeme katika treni hiyo,Nyamohanga amesema mradi huo una line maalumu ya umeme na shida ilikuwa ni mfumo kutumika kwa mara ya kwanza hivyo walikuwa wakijifunza jinsi ya kuendesha.

“Kitu kinapokuwa kipya kinaleta shida niwahakikishie watanzania ile line ipo madhubiti na inaendelea kuimarika,”amesema Mkurugenzi huyo.

Kuhusu kukatikatika kwa umeme nchini , Mkurugenzi huyo Mtendaji amesema sababu kubwa ni kuzidiwa kwa gridi ya Taifa kutokana na ongezeko la watumiaji wa umeme huku akidai Shirika limejipanga kuhakikisha umeme unapatikana katika kila eneo nchini.

Hata hivyo amesema Shirika linajipanga katika matumizi ya tehama pindi Mteja atapanunua tokeni apate umeme moja kwa moja tofauti na sasa ambapo hupata tokeni.

Kuhusu Tanzania kununua umeme kutoka nje ya Tanzania amesema sababu kubwa ni za Kijiografia kutokana na maeneo ya pembezo kuwa magumu kufikika katika suala la miundombinu.

“Mtu anakaa Sumbawanga anaona umeme Zambia unawaka kama Taifa tukasema tuweke mipango badala ya kuawaacha waendelee kuteseka tuchukue umeme tuwalipe lengo ni wapate umeme kwanza,”amesema Nyamohanga.

Hata hivyo amesema Shirika hilo limejipanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2027 watanzania wote wanatumia umeme wa ndani ikiwemo maeneo ya pembezoni.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.