Na Mwandishi Wetu
Tamasha kubwa la kuombea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 linatarajiwa kuanza rasmi Juni 21, 2025 jijini Dar es Salaam, likihusisha waimbaji wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Tamasha hilo litaendelea katika mikoa yote 26 ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Msama Promotions na muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, amesema lengo kuu ni kuliombea taifa libaki katika hali ya amani, upendo na usalama hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
“Tamasha ni sehemu nzuri ya kuliombea taifa letu. Tunamuomba Mungu atupatie viongozi walioteuliwa na yeye mwenyewe – viongozi wa haki, wenye maono na hofu ya Mungu,” alisema Msama.
Amebainisha kuwa tayari mazungumzo yamekamilika na baadhi ya waimbaji kutoka mataifa mbalimbali, ikiwemo Afrika Kusini na Nigeria, huku mazungumzo yakiendelea na waimbaji kutoka Rwanda. Waimbaji wa ndani ya nchi nao wamejiandaa kushiriki tamasha hilo.
Msama pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini tamasha hilo kutokana na gharama kubwa za kuandaa na kuwaleta waimbaji kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wake, Askofu Resambulo Mlaki amesema ni wakati muhimu kwa waumini na Watanzania kwa ujumla kumuomba Mungu alilinde taifa kuelekea uchaguzi huo muhimu.
Naye Mchungaji Philip Mwotsi wa Kanisa la FPCF, amesema maombi ni silaha muhimu ya kulinda taifa na kuhakikisha viongozi wanaopatikana wanatokana na mapenzi ya Mungu.
Mchungaji Rose David kutoka Kanisa la Pentekoste ameongeza, “Watanzania tuungane kwa maombi kuelekea uchaguzi mkuu. Wito wangu ni kwa akina baba na mama kujitoke
Crédito: Link de origem