Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea uchaguzi mkuu 2025 ndugu Alex Msama amesema Maandalizi ya Tamasha la kuombea uchaguzi yanaendelea vizuri na kuwa Tamasha hilo litafanyika mwezi, Aprili 2025 katika jiji la Dar es Salaam na baadae kufanyika Mikoa 26 ya Tanzania.
Hayo ameyasema leo alipongea na waandishi wa Habari kuhusiana na maandalizi ya Tamasha hilo kwa kusema kuwa “Maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na tunakaribisha wadhamini kuja kusaidia kufanikisha Tamasha hili kubwa ambalo litafanyika Mikoa yote ya nchi yetu ya Tanzania tukianzia na Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha Msama amewaomba watanzania kuhudhulia tamasha hilo kwani kufika kwao ni utimilifu wa tukio, pia amewataka wasanii wa injili kutumia tamasha hilo kama fursa ya kuonesha vipaji vya na kujitambulisha kwa watanzania kupitia tukio hilo.
Ndugu Alex Msama Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya tamasha hilo amesema kwasasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili na tukifanikiwa tu kupata wadhamini basi tamasha litakuwa halina kingilio litakuwa bule.
Tamasha la Kuombea uchaguzi litafanyika hivi karibuni na lengo kuu ni kuwaunganisha waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili Ndani na Nje ya Tanzania.
Crédito: Link de origem