top-news-1350×250-leaderboard-1

Sababu wanawake kudanganya wakati wa tendo la ndoa

Kufika kileleni ni msisimko wa kipekee, unaoleta hisia nzuri kwa wenza wawili wanaowajibika kikamilifu katika tendo la ndoa.

Hisia hizi hutokea kwa wenza ambao ni mke na mume wote kama ishara ya kufikia kilele cha tendo hilo adhimu ambalo ni sababu ya uumbaji.

Hisia hizo huambatana na mtiririko wa matukio yanayohusisha mfumo wa fahamu (ubongo na mishipa ya neva), damu na moyo na maeneo mengineyo ikiwamo viungo vya uzazi.

Wenza wanapofika kwenye mshindo, mapigo ya moyo hubadilika, hudunda kwa haraka huku upumuaji ukiwa ni wa kasi na kuvuta pumzi kwa nguvu.

Kwa wanawake, hali hii huwa ni nzito na ya kipekee. Kufika kwao kileleni na kupata hisia nzuri, huambatana na kujikunja ama kujikaza kwa misuli ya maeneo ya sehemu nyeti, nyumba ya uzazi na kiunoni.

Wataalamu wa afya wanasema mwanamke anaweza kufika kileleni zaidi ya mara moja muda mfupi tu tangu alipofika kileleni mara ya kwanza, na ataendelea kupata hisia hizo endapo ataendelea kusisimuliwa, hisia hizi hudumu kwa sekunde 15 hadi 60.

Utafiti uliochapishwa kupitia jarida liitwalo Journal of Sex Research ya nchini Marekani, umebaini wanawake huwadanganya wapenzi au waume zao kuwa wamefika kileleni ilihali hawajafika.

Uchunguzi huo wa kitabibu uliofanyika kwa nchi za Ulaya, watafiti wake wanaeleza sababu za uongo huo kwa wanawake unachangiwa na wahusika kuwa na wapenzi wengi, kuwa na watoto au kuwa na tabia ya kushiriki mapenzi ya jinsi moja.

 Aidha, utafiti huo uligundua watu ambao wapo kwenye uhusiano unaofahamika, ndio walikuwa na tabia ya kudanganya kufika kileleni.

 Pia kundi hilo la wanawake inaelezwa kupitia utafiti huo, wanapitia msongo wa mawazo kwa mambo mbalimbali wanayokumbana nayo katika kipindi cha maisha yao.

 Wanaume na wanawake ambao walikuwa na tabia hiyo kupitia utafiti huo, walieleza sababu ya kuwa na tabia hiyo.

 “Tuligundua kudanganya kufika kileleni kulihusiana na kuridhika kidogo na masuala ya ngono, uhusiano na maisha kwa ujumla.

 Utafiti uliofanywa awali ulionyesha kibaiolojia wanawake wakati mwingine, hupata ugumu wa kufikia kilele wakati wa mapenzi.

 “Tunaamini kuwa katika suala la wapenzi kufika kileleni wakishiriki ngono, mazungumzo ni jambo muhimu sana,” anasema Dk Silvia wa Chuo Kikuu cha Copenhagen.

Wanasaikolojia wanasemaje?

Akizungumzia utafiti huo, Mtaalamu wa saikolojia Radhamani Masenga anasema tendo la ndoa kwa mwanaume, ni sehemu ya kuonyesha uimara wake na thamani yake.

“Mwanaume ambaye hawezi kukidhi haja ya mwanamke anajiona mnyonge, asiye na thamani mbele ya mwanamke…wanawake wana uwezo mkubwa wa kutambua hali hiyo ya mwanaume,”anasema.

Anasema tafiti mbalimbali zinaonyesha wanawake kwa asilimia 72 wanaodai wanafika kileleni wengi wao hawafiki, lakini wanaume wanamini wanawafikisha wenza wao kileleni.

 Mtaalamu huyo anasema mwanamke anafahamu kuwa kumweleza mwanaume kuwa hajamridhisha, kutamfanya ajisikie vibaya na hata hivyo anasema wanaume hawawezi kumudu kauli hiyo wanapoambiwa.

“Wanaume wengi hawana uwezo wa kuhimili maneno ya wanawake wanapoambiwa wameshindwa kuwafikisha kileleni,”anasema.

Anasema mwanaume anapoambiwa hawezi kumridhisha mkewe au mpenzi wake, huanza kulaumu kuwa yapo mambo mpenzi au mke hufanya ndio sababu hafiki kileleni.

Kutokana na hofu ya kusemwa na kuachwa Masenga anasema wanawake hukiri kufika kileleni lakini ukweli hawafiki.

“Tatizo linaendelea kuwepo na wanawake wanaanza kutafuta njia nyingine za kukidhi mahitaji yao ama kwa kutumia vyombo bandia, wakati mwingine wanalazimika kusema uongo kwasababu hawapo kwenye uhusiano huo kutokana na mapenzi bali kutafuta fedha,”anasema.

Irene Steven mkazi wa Tabata amesema wanawake huchelewa kufika kileleni wakati mwingine kutokana na mandalizi ya mwanaume.

“Badhi ya wanaume hawawaandai wapenzi wao wanapoingia kwenye tendo la ndoa, anakutana na mwanamke hata dakika 30 ya maandalizi hakuna dakika tano nyingi ameshamaliza,kwa hatua hiyo ni ngumu kumfikisha mwenza kileleni,”anasema.

Irene anasema ili kutosababisha mtafaruku, mwanamke huridhika na kile kilichofanyika na humsifia mpenzi wake lakini ukweli mwanaume wa namna hivyo anapomaliza hisia zake, ndipo mwanamke naye huanza.

 Naye John Isaya mkazi wa Mbezi Dar es Salaam anasema suala la kufikisha wanawake kileleni ni mjadala usioisha kwani matatizo yanachangiwa na pande zote mbili.

“Unakuta mtu anadaiwa vikundi, sherehe kila mahali anataka aishi maisha yasiyo yake sasa huyu ukikutana naye atataka mmalizane haraka aendelee na shughuli zake. Hakuna maandalizi wala muda wa kutosha wa kutengeneza hisia zaidi,”anasema.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.