Na Mohammed Ulongo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi quran tukufu yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 mwezi huu.
Hayo yamebainishwa Mapema hii leo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo Mkurugenzi wa taasisi ya Bi Aisha Sululu Foundation, Bi.Aisha Sululu amesema mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilii jijini Dar es salaam.
Aidha Bi Aisha Sululu amesema mashindano haya yamejumuisha mikoa yote ya Tanzania ikiwemo ya visiwani unguja na pemba hivyo amewataka watanzania kujitokeza kushuhudia mashindano hayo katika ukumbi wa diamond jubilii.
Kwa upande wake Sheikh Othmani Kaporo pia amewataka watanzania kuhudhulia katika mashindano hayo kwani kufanya hivyo ni kutambua thamani ya mwezi mtukufu na quran pamoja na kumtia nguvu mwanamke pekee anayeandaa mashindano ya quran katika nchi ya Tanzania.
Katika hatua nyingine sheikh kaporo amewataka watanzania kujitokeza katika mashindano ya quran ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika tarehe 16 mwezi huu mashindano ambayo yanaandaliwa na sheikh Nurdin Kishki, mwenyekiti wa taasisi ya Al hikma Foundation.
Crédito: Link de origem