top-news-1350×250-leaderboard-1

Polisi Dar kuimarisha ulinzi, usalama Sikukuu ya Idd

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam limesema limejipanga kuhakikisha waumini wa Kiislamu wanashiriki na kusherehekea Sikukuu ya Eid al-Adhaa kwa amani na utulivu.

Sikukuu hiyo huhusisha ibada mbalimbali katika nyumba za ibada na maeneo ya wazi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 6, 2025 na Kamanda Kanda Maalumu, Jumanne Muliro na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu kwa watoto wakati wa matembezi na mikusanyiko mbalimbali, pia nyumba na makazi yasiachwe bila uangalizi wakati wa sherehe hiyo.

Suala la usalama barabarani amewasisitiza  madereva wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia sheria ili kuepusha ajali. 

“Jeshi linawatakia sikukuu njema ya Eid al-Ad ha wananchi wote wa Dar es Salaam wanaoungana na Watanzania wenzao,” amesema Kamanda Muliro.

Hata hivyo kwa mujibu wa mwandamo wa mwezi, Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) lilitangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Adh’haa itakuwa Juni 7, 2025 na itaadhimishwa kitaifa jijini Dar es Salaam.

Sikukuu hii imeanza kuadhimishwa leo Ijumaa katika baadhi ya mataifa, huku wengine wakingojea kuiadhimisha kesho, Juni 7, 2025.

Kwa mujibu wa DW, karibu Waislamu bilioni 1.9 kote ulimwenguni ambao ni sawa na asilimia 25 ya idadi ya watu, wanasherehekea sikukuu hii ya Idd baada ya kukamilisha ibada ya Hijja mojawapo ya nguzo tano za Uislamu. Pia kwenye sikukuu hii Waislamu huandaa kuanzia makazi yao, kununua mavazi mapya na kuandaa vyakula maalumu kwa ajili ya kusherehekea.

Katika siku ya kwanza ya sikukuu hii, wale wanaojiweza kifedha hutakiwa kutoa sadaka ya wanyama ambayo huwa ni kondoo, mbuzi, ng’ombe au ngamia na kuwagawia wasiojiweza sehemu ya sadaka hiyo. Kitendo hicho hurejesha kumbukumbu ya Nabii Ibrahim kumtoa kafara mwanawe wa kiume Ismail kwa utiifu mkubwa kwa Mwenyezi Mungu.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.