Dar es Salaam. Mwalimu wa Shule ya Msingi Kilulu, iliyopo wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, Emmanuel Pamba Everist, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili.
Mwalimu huyo amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu, baada ya kupatikana na hatia kwa makosa ya kughushi nyaraka na kujiongezea umri kwa lengo la kuonesha kuwa amefikisha umri wa kustaafu kwa hiyari.
Kwa njia hiyo, alifanikiwa kujipatia fedha za mafao ya kustaafu ilhali bado alikuwa anaendelea na kazi.
Amehukumiwa adhabu hiyo na Hakimu Martha Mahumbuga, baada ya kupatikana na hatia katika makosa sita yaliyokuwa yakimkabili.
Katika hukumu hiyo, makosa matano yalimhukumu kifungo cha miaka saba kwa kila kosa, huku kosa moja likimpelekea kuhukumiwa kifungo cha miaka 30.
Hivyo, katika hukumu hiyo iliyotolewa Mei 7, 2025, am-bayo Gazeti la Mwananchi limeiona nakala yake jana, Alhamisi Mei 29, 2025, mwalimu huyo atalazimika kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, kwa kuwa adhabu zote zitaendeshwa sambamba (concurrently).
Hata hivyo, wakati mwalimu Pamba akitiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hiyo, mwenzake aliyeshtakiwa pamoja naye, Zephania William, ambaye alikuwa Ofisa Rasilimali Watu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi (Sikonge), aliachiwa huru baada ya mahakama hiyo ku-baini kuwa hana hatia katika mashitaka yaliyokuwa yakimkabili.
Akizungumzia hukumu hiyo, hasa mshtakiwa wa pili, William kuachiliwa huru, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Simiyu, Manyama Tungaraza amelieleza Mwananchi, leo Jumatano, Mei 28, 2025 kuwa hawatamkatia rufaa na kwamba wameridhika na hukumu hiyo.
Tungaraza amesema kuwa kwa mujibu wa Mwanasheria wao aliyehusika kuendesha kesi hiyo, kutokana na uchambuzi wa mahakama wa ushahidi dhidi ya mshtaki-wa huyo wamekubaliana na uamuzi wa mahakama.
“Kwa hiyo hatukusudii kuchukua hatua yoyote maana tumeridhika na hukumu hii,” amesema Tungaraza.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za kesi hiyo, Mwalimu Pamba na William walikula njama na kughushi nyaraka mbalimbali na mihuri kwa kushirikiana na Ofisa Uzingati-aji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mohamed Seleman Nyangi, am-baye alikuwa hajakamatwa.
Mwalimu Pamba na William walidaiwa kuwa waligu-shi Fomu ya Maombi ya Mafao ya Kustaafu, kwa ku-shirikiana na
Fomu hiyo ilienga kuonesha kuwa Mwalimu Pamba alikuwa amefikia umri wa kustaafu kwa hiyari na kwam-ba anastahili mafao yaliyoombwa.
Pia, Mwalimu Pamba alidaiwa kughushi Risiti ya Malipo ya Mshahara (salary slip) kuonesha kuwa ni halisi na imetolewa na Wizara ya Fedha na Mipango na ilipakiwa kati-ka Mfumo wa Malipo ya Mishahara (Salary Slip Portal).
William alidaiwa kusaini kibali cha kustaafu kazi kwa hiyari, cha Novemba 24, 2021, kilichokusudia kuonesha kuwa ni taarifa halisi ya kustaafu iliyotolewa na mwajiri wa Mwalimu Pamba, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Pia, William alidaiwa kusaini barua ya kubadilisha tarehe ya Kuzaliwa iliyokusudia kuonesha kuwa ilikuwa halisi ya na kwamba ilikuwa imetolewa na/kwa niaba ya Mku-rugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Nyangi alibadili tarehe ya kuzaliwa ya Mwalimu Pamba, kutoka Juni 30, 1968 na kuwa Aprili 26, 1967.
Hata hivyo, kwa mujibu wa vielelezo mbalimbali na kwa ushahidi wake mwenyewe Mwalimu Pamba alizaliwa Septemba 2, 1968.
Hivyo Mwalimu huyo alikuwa amebakiza mwaka mmoja, miezi mitano na siku 24 kufikia umri wa miaka 55 ya kustaafu kwa hiyari.
Hakuweza kuvumilia kusubiria muda huo ufike badala yake akaamua kujiongezea muda huo uliokuwa umesalia.
Kisha Mwalimu Pamba aliwasilisha katika ofisi za PSSSF, Bariadi, Simiyu, nyaraka hizo kikiwemo kibali hicho cha kustaafu kazi wa hiyari, pamoja na risiti hiyo ya malipo ya mshahara (aliyoighushi), hatimaye akalip-wa Sh70,317,644,.44 (zaidi ya Sh70.3 milioni) kama mafao yake ya kustaafu.
Hata hivyo, aliendelea kufundisha shuleni hapo akilipwa mshahara na kukatwa michango ya hifadhi ya jamiii kila mwezi ambayo iliendelea kuwasilishwa PSSSF.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Takukuru, Aprili 14, 2024, Mwalimu Pamba na William walipandishwa ki-zimbani.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 9350 ya mwaka 2024,wote kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane, wakidaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofautitofauti kati ya Aprili 20, 28, 30, Mei 30 na Juni 12, 2022.
Mwalimu Pamba alikuwa anakabiliwa na jumla ya mashtaka sita, mashtaka manne ya peke yake ambayo yalikuwa ni shtaka mawili la kughushi, mawili ya kuwasi-lisha nyaraka za uwongo na moja la kujipatia pe-sa, Sh70,317,644.44, kwa udanganyifu.
William kwa upande wake alikuwa anakabiliwa na jumla ya mashtaka manne, mawili ya peke yake, yote ya ku-ghushi, huku wote wawili wakikabiliwa na mashtaka ya pamoja mawili, la kughushi na la kuisababishia hasara mamlaka ( PSSSF),Sh70,317,644.44.
Mwalimu Pamba katika utetezi wake alikiri kuzaliwa Sep-temba 2, 1968, na kwamba bado alikuwa anafundisha katika Shule ya Msingi Kilulu, akipokea mshahara na michango yake kuwasilishwa PSSSF kila mwezi
lakini alikana mashtaka kula njama na mshtakiwa wa pili kutenda makosa waliyoshtakiwa.
William yeye pamoja na mambo mengine, pia alikana mashtaka hayo akidai kuwa kati ya Februari 24,2022 na Machi 6,2023 alisimamishwa kazi, hivyo wakati huo waliodaiwa kutenda makosa hayo yaani kati ya Aprili, 2022 na Juni 12,2022 hakuwepo kazini.
Hakimu Mahumbuga katika hukumu yake amekubaliana na upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake tisa ku-wa umeweza kuthibitisha mashtaka yote dhidi ya Mwa-limu Pamba. Hivyo alimtia hatiani na kumhukuku.adhabu hiyo.
Hata hivyo, Hakimu Mahumbuga amesema kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa wa pili, William. Hivyo amesema kuwa hana hatia kwa makosa aliyokuwa alishtakiwa na aliamuru aachiliwe huru.
Crédito: Link de origem