top-news-1350×250-leaderboard-1

Miji hii kwa kunguni usipime

Washington. Wakati msimu wa kiangazi ukikaribia kuanza katika mataifa ya Amerika na Ulaya, taasisi ya Terminix inayojihusisha na kupambana na wadudu nchini Marekani limeanika majiji kinara kwa uwepo wa Kunguni.

Kunguni ni mdudu mdogo anayesifika kutokana na usumbufu wake kwa binadamu hususan kutokana na tabia yake ya kung’ata, kuwa kero wakati wa kulala na kusambaa kwa kasi katika mazingira hususan ni kwenye makazi.

Miongoni mwa njia zinazotajwa kusababisha kusambaa kwa wadudu hao wanaotajwa kuwa kero hadi barani Afrika ni pamoja na muingiliano wa watu katika miji na majiji hususan ni wanaofanya hivyo kwa lengo la kufanya shughuli za kitalii.

Marekani ni miongoni mwa mataifa yaliyokumbana na changamoto ya kunguni kwa kiwango cha juu wakati wa mlipuko wa Uviko-19 baadaye taifa hilo lilitangaza kuwadhibiti kwa kiwango kikubwa hata hivyo, Terminix imeibua taarifa mpya ya kuibuka kwa waduu hao.

Taasisi ya Terminix imetoa orodha yake ya kila mwaka ya miji 50 yenye shida kubwa zaidi ya kunguni nchini Marekani huku ikiwataka wananchi wanaotarajia kusafiri na kubadilisha mazingira msimu huu wa kiangazi kuwa makini ili kutowakaribisha wageni (kunguni) kwenye makazi yao.

Kwa kutumia takwimu za huduma kutoka kwa matawi zaidi ya 300 kote nchini Marekani, Terminix imeitaja miji 50 bora iliyohitaji huduma za kudhibiti kunguni katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Meneja wa Huduma za Kiufundi katika kampuni ya Terminix, Eric Braun amesema kuna ongezeko la kasi la huduma za kudhibiti wadudu hapo huku baadhi ya miji na majiji yakiihitaji kwa kiwango kikubwa.

“Tumeona ongezeko la mara kwa mara la huduma za kudhibiti kunguni tangu maisha yarejee kwenye hali ya kawaida toka kutokee mlipuko wa Uviko-19,” amesema Braun.

Braun ameutaja Mji wa Philadelphia kuwa kinara kwa kushika nafasi ya kwanza mara mbili mfululizo wa kuhitaji huduma ya kupambana na kunguni ikifuatiwa na New York na Cleveland-Akron ambazo zimeingia tano bora, jambo linaloonesha ongezeko la changamoto ya wadudu hao sugu.

Majimbo yaliyoonekana mara nyingi zaidi ni Ohio, Texas, Florida, California, na Pennsylvania, ikionyesha kuwa kusambaa kwa wadudu hao kunaweza kuhusishwa na hali ya hewa, mwenendo wa makazi, na vituo vya usafiri.

Braun amewataka wakazi wa miji ama wanaotembelea miji hiyo kuhakikisha wanakagua sehemu za godoro, kichwa cha kitanda, na samani za ndani na iwapo watabaini uwepo wa madoa madogo ya kutu, ngozi zinazoning’inia, ama kunguni walio hai.

Amesema Kunguni waliokomaa wana ukubwa wa punje ya mbegu ya tofaa, hivyo akawataka kuangalia kwa makini.

“Tumia tochi (ya simu yako) kuchunguza kona na mikunjo ya kina, Angalia pia meza za kando ya kitanda, pembe za viti au sofa, na sehemu za viungio vya droo. Usihifadhi mzigo wako juu ya kitanda au sakafu unapokagua chumba,” amesema Braun.

“Wakati wa kusafiri, funga begi lako kila wakati na fikiria kuliweka kwenye mfuko mkubwa wa plastiki uliofungwa. Unaporudi nyumbani, fungua mzigo wako juu ya sehemu ngumu (si sakafu yenye zulia au kitandani), mbali na chumba cha kulala mfano: sehemu ya nje au gereji ili kuepuka kuwasambaza (kama unao kwenye begi),” amesema.

Pia ameshauri kuvaa nguo zilizofuliwa na kunyooshwa kwa kutumia mashine za kufulia na kukaushia nguo kwa pasi kwa angalau dakika 30, kwa kile alichodai wadudu hao hudhurika na mayai yao endapo yataunguzwa kwa maji ya moto kwa dakika angalau 30.

“Unaporudi nyumbani, fungua begi lako nje au wenye sehemu kama gereji ili kuepuka kuwaleta kunguni kwenye maeneo ya kulala. Kwa kuchukua hatua chache za tahadhari, unaweza kujilinda dhidi ya kuwaleta kunguni bila kujua,” amesema Braun.

Kuhusu ambao tayari wanaishi na Kunguni kwenye makazi yao, Braun ameshauri kufanyika jitihada za kuzuia wasiendelee kuenea.

“Epuka kuhamisha vitu vilivyoathirika kati ya vyumba kwani hiyo inaweza kusambaza tatizo. Jiepushe na dawa za kunyunyizia za dukani, kwani kunguni wengi wamekuwa sugu kwa dawa hizo na zinaweza kuwafanya wasambae zaidi.”

“Kuchukua hatua mapema kunaweza kusaidia kupunguza athari kabla ya matibabu ya kitaalamu kufanyika,” amesema.

Orodha ya miji na majiji 50 yenye kunguni zaidi, kulingana na idadi ya matibabu yaliyofanyika kama ilivyoripotiwa na taasisi ya Terminix ni:

    •  Philadelphia

    •  Cleveland-Akron (Canton)

    •  Dallas – Ft. Worth

    •  Washington, D.C (Hagerstown)

    •  San Francisco – Oakland – San Jose

    •  Indianapolis

    •  Boston (Manchester)

    •  Oklahoma City

    •  Little Rock – Pine Bluff

    •  Tampa – St. Petersburg (Sarasota)

    •  Charleston – Huntington

    •  Orlando – Daytona Beach – Melbourne

    •  Sacramento – Stockton – Modesto

    •  Fort Smith – Fayetteville – Springfield – Rogers

    •  Richmond – Petersburg

    •  Wichita – Hutchinson

    •  Miami – Ft. Lauderdale

    •  Paducah – Cape Girardeau – Harrisburg

    •  Harrisburg – Lancaster – Lebanon – York

    •  Hartford & New Haven

    •  Tyler – Longview

    •  Champaign & Springfield-Decatur

    •  Roanoke – Lynchburg

    •  Palm Springs

    •  Montgomery (Selma).

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.