top-news-1350×250-leaderboard-1

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Mapato Tanzania Updates – Jobs in Tanzania

TRA: Vituo na Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA Updates
TRA:
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Mapato Tanzania Kutoka
KeshoMkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania
(TRA) Bw. Moshi Jonathan Kabengwe amesema majina ya waombaji wa ajira
1,596 za TRA zilizotangazwa hivi karibuni yatatangazwa rasmi Machi
22.2025 kupitia tovuti ya tra.go.tz na hapa www.ajiraleo.com kwa ajili ya usaili wa kuandika
utakaofanyika Machi 29 na 30 mwaka huu kwenye vituo 9.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo tarehe
21.03.2025 Bw. Kabengwe amesema kati ya waombaji 135,027 waliotuma
maombi ya nafasi za ajira, waombaji 112,952 wamekidhi vigezo na kuitwa
kwenye usaili wa kuandika.

Amesema kila muombaji atatumiwa
taarifa ya kuitwa kwenye usaili katika barua pepe yake aliyoiambatanisha
kwenye maombi ya kazi na kuwa waombaji wenye mahitaji maalum wamewekewa
utaratibu maalum ambao utawasaidia kufanya usaili bila usumbufu.

Vituo vya Usaili TRA kwa Watakaoitwa kwenye Interview Mamlaka ya Mapato TanzaniaLeo

Bw. Kabengwe amesema usaili huo utafanyika kwenye Mikoa 8 na Zanzibar ambayo ni:
1. Dar es Salaam ambayo itahusisha waombaji kutoka Dar es Salaam na
Pwani.

2. Zanzibar ambayo itahusisha waombaji kutoka Unguja na Pemba

3. Arusha ambayo itahusisha waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga

4. Dodoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora

5. Mtwara ambayo itahusisha waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma

6. Mbeya ambayo itahusisha waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa

7. Mwanza ambayo itahusisha waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu

8. Kagera ambayo itahusisha waombaji kutoka Kagera na Geita na

9. Kigoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Kigoma na Katavi.
Endela kurembelea page hii ili uwe wa kwanza kuona majina punde tu yatakapotoka mdau!

logoblog





Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.