Dodoma. Mkutano Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi umemchagua Haji Khamis kuwa mwenyekiti wa chama hicho akichukua nafasi ya James Mbatia aliyekuwa mwenyekiti.
Wajumbe wa mkutano huo wamemchangua Khamis kwa kura 508 kati ya kura 511, huku kura moja ikimpinga na mbili ziliharibika.
Khamis alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar na muda mrefu amekuwa akikaimu nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho baada kuondolewa James Mbatia.
Mkutano Mkuu wa NCCR Mageuzi umefanyika leo Jumamosi Machi 29, 2025 jijini Dodoma ambapo mbali na uongozi wa kitaifa, pia kulikuwa na uchaguzi wa ngazi zingine za uongozi.
Pia, katika uchaguzi huo Joseph Selasini ametetea nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Tanzania (Bara) baada ya kupata kura za ndiyo 483, huku 12 ziliharibika na 16 zikimtaaa.

Kabla ya uchaguzi wa leo Selasini alikuwa Makamu Mwenyekiti na ndiye aliyeongoza mageuzi ya uongozi ndani ya chama hicho kikongwe cha upinzani.
Kwa upande wa Makamu wa Tanzania Zanzibar nafasi hiyo amechukua Laila Rajabu Khamisi ambaye alipata kura za ndiyo 478 na kura zilizomkataa zilikuwa 15 wakati 18 ziliharibika.
Nafasi nyingi zilizokuwa zikigombewa leo zilikuwa na mtu mmoja mmoja na hivyo wajumbe walikuwa wakipiga kura za ndiyo na hapana
Crédito: Link de origem