top-news-1350×250-leaderboard-1

Haloteli yazindua kampeni ya kuchangia damu, kumsaidia mama na mtoto

Na Iman Nathaniel, Dar es Salaam

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, imezindua Kampeni maalum ya kuchangia damu ikishirikiana na Kitengo cha Damu Salama nchini lengo likiwan kumsaidia mama na mtoto na wagonjwa wengine wa dharura.

Uzinduzi huo uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam, ni mpango wa kampuni hiyo wa kuhudumia jamii na kuongeza ufahamu wa umuhimu wa kuchangia damu katika vyuo mbalimbali jijini.

Akizungumzia kampeni hiyo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Halotel, Abdallah Salum amesema kwa kushirikiana na kitengo cha damu salama, wanataka kuwapa nguvu wahitaji wa damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto, pia wagonjwa wengine wa dharura hasa waathirika wa ajali.

Mkurugenzi huyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi katika maeneo husika ili kusaidia kuokoa maisha ya wahitaji wa damu.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Roxana Kadio, amesema kampuni ya Halotel inajukumu la kuungana na jamii katika masuala mablimbali ikiwamo hili la kuchangia damu, wakiamini ni moja ya sadaka.

Naye Ofisa Mhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama , Joel Temba, amesema kampeni hiyo ina lengo la kukusanya damu kwa ajili ya kumnyanyua mama na mtoto kitandani ambapo ameomba kila familia ijitokeze kwa ajili ya kuweka akiba ya damu ili iweze kuokoa watu wenye changamoto nchini.

Kwa upande wao wafanyakazi wa WOISO Production walioshriki katika zoezi hilo wamesema uchangiaji wa damu ni sadaka ambayo kila mtu anatakiwa kuchangia kwani ni akiba ambayo inaokoa na kuhuisha tena maisha ya watu.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.