Imani Nathaniel, Mtanzania Digital
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel,imezindua huduma mpya itakayosaidia mteja kujihudumia kwa kutoa taarifa juu ya jambo alilolitilia mashaka ilikupunguza changamoto ya mawasiliano kati ya mtoa huduma na mteja.
Mbali na jambo hilo huduma hiyo pia inatoa nafasi kwa mteja kuangalia salio, kununua vifurushi na huduma nyingine.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Machi 20,2025, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Halotel, Abdallah Salum, amesema huduma hiyo inayofahamika kwa jina la ‘Miss Halo’ imeziduliwa ili mteja aweze kuwasiliana na kampuni kupitia kitengo cha huduma kwa wateja moja kwa moja.
“Tunajua tulikuwa tukiwasiliana na wateja wetu kupitia namba 100 au mteja kufika ofisini na kueleza shida yake na baadae kutatuliwa,lakini kupitia huduma hii mpya mteja wetu ataweza kujihudumia mwenyewe bila shida kwani atatumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram pamoja na Whatsapp kwa namba 0620100100.

“Kwa sasa dunia inaenda kidigitali hivyo na sisi kama kampuni ya mawasiliano ni lazima twende na teknolojia ya kutumia akili mnemba ili kupunguza ama kuondoa kabisa masuala ya utapeli mitandaoni,ni wambie tu wateja wetu huduma hii inazingatia na kutunza taarifa za mteja,” amesema.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa wateja Halotel, Shabani Said, amesema kuwa kadri sekta ya mawasiliano inashuhudia mageuzi kuna umuhimu wa ubunifu na ufanisi ambapo Miss Halo ni njia ya kuhakikisha wateja wanapata msaada wa kwa haraka.

Amesema kwa sasa sekta ya mawasiliano imekuwa na mageuzi makubwa hivyo ni lazima kuwa na ubunifu na ufanisi hili kuhakikisha wateja wanapata msaada wa haraka na wa kuaminika.
Amesema huduma hiyo itaendelea kutatua matatizo ya kawaida na kutoa majibu moja kwa moja na kupunguza muda wa kusubiri kwani imerahisishwa kwa lugha ya kiingereza na kiswahili.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Halotel, Roxana Kadio amesema kampuni hiyo inaendelea kuimarisha sifa yake kama chapa inayojali wateja kwa kutoa sio tu huduma bora za mawasiliano bali uzoefu unaoboresha maisha ya watumiaji wake hivyo jamii itumie huduma hiyo kwani ni rahisi .
Crédito: Link de origem