top-news-1350×250-leaderboard-1

Halotel yaadhimisha Siku ya Wanawake kwa kuwapatia usafiri wa baiskeli wanafunzi Shule ya Sekondari Visiga

Na Imani Nathanieli, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel imedhibitisha dhamira yake katika uwajibikaji Sekata kwenye jamii baada ya kuwapatia usafiri wa baiskeli wanafunzi wa shule ya Sekondari Visiga iliyoko mkoani Pwani ikiwa ni moja ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Lengo la kufanya hivyo ni kutatua changamoto wanazokumbana nazo wanafunzi katika elimu, hivyo Halotel imetoa baiskeli zinatakazoweza kutumika kwa muda mrefu ambapo mpango huo ni kuwajengea ujasiri wanafunzi na kusisitiza umuhimu wa kuwahi shule.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kugawa baiskeli hizo, Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Abdul Salim, amesema kuwa juhudi hiyo ni moja ya dhamira pana ya kuwawezesha wanafunzi kutambua kuwa wanaweza kuendelea na masomo bila vikwazo visivyo vya lazima.

” Kwa kuwaunga mkono hawa tunatarajia kuleta athari chanya za kudumu katika maisha yao na kuwahamisha kufikia uwezo wao kamili” amesema Abdul.

Naye Ofisa wa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma , Roxana Kadio, amesema kampuni ya Halotel imetoa msaada huo ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hivyo Halotel imeona ni vema kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa kutoa msaada katika shule hiyo.

Kwa Upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Visiga, Aurelian Njau, amesema kuwa ni jambo la kiungwana lililofanywa na Halotel kwani wameweza kurudisha shukrani kwa jamii ambayo wanaihudumia hivyo ameziomba na tassisi nyingine kuiga walichokifanya.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wa wanafunzi, Maria Lau, amesema kuwa msaada huo ni muhimu utawasaidia watoto wao kuwahi shuleni na nyumbani na itasaidia kuwafanya wajikite zaidi katika masomo.

Aidha kupitia mpango huu wa uwajibikaji wa Kijamii (CSR), Halotel inaendelea kuimarisha nafasi yake ya kama mshirika wa kuaminiwa katika maendeleo ya jamii, ikifanyakazi kuelekea jamii jumuishi na yenye msaada kwa wote .

Kampuni inabaki kujitolea kuinua jamii kupitia program mbalimbali zinazolenga elimu ,jumuishi ya kidigitali na uwezeshaji wa kijamii.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.