Na Nora Damian, Mtanzania Digital
Katibu Mkuu wa Chama cha National for League Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, amechukua fomu kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza leo Machi 20,2025 wakati wa kuchukua fomu hiyo amesema endapo chama chake kitaridhia na kumpa jukumu hilo atajitahidi kuleta mapinduzi katika sekta za afya, elimu, uchumi na utawala.
Aidha amesema kaulimbiu ya uchaguzi mkuu ya chama hicho ya ‘Uzalendo, haki na maendeleo’ ina maana kubwa kwa sababu inakwenda kuibeba nchi katika uzalendo, kushughulikia masuala ya haki na kuhakikisha nchi inakuwa na maendeleo.
“Nawaomba Watanzania tusiishi lwa mazoeya, funahitaji mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kiuongozi katika taifa letu hivyo hatupaswi kuchagua viongozi kwa mazoeya au kwa ukubwa wa majina yao au vyama vyao.
“Mtu yeyote anaweza kugombea urais si lazima atoke kwenye chama kikubwa cha siasa, ‘idea’ ya uongozi inatoka katika fikra chanya kwa mwanadamu yeyote ili mradi ana akili timamu na uelewa wa kitu anachokifanya…mimi naelewa ninachokifanya.
“Endapo nitapitishwa na chama na kuwa mgombea rasmi nitakwenda kupambana ili kushinda ili tukabadilishe maisha na mifumo ya Watanzania,” amesema Doyo.
Naye Mwenyekiti wa kigoda cha Wazee NLD Taifa, Tozi matwanga, amempongeza Doyo na kusema anatosha kuwania urais kwa kuwa ni timamu, shupavu na anayeiweza nafasi hiyo.
Crédito: Link de origem