top-news-1350×250-leaderboard-1

Bahati Nasibu ya Taifa yaungana na Mixx by Yas kuelekea uzinduzi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Bahati Nasibu ya Taifa Tanzania imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Mixx by Yas, hatua muhimu inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma zake sokoni kuelekea uzinduzi rasmi unaosubiriwa kwa hamu kubwa.

Ushirikiano huu unalenga kuhakikisha kuwa wateja wa mtandao wa Yas Tanzania, wenye zaidi ya watumiaji milioni 23, wanapata fursa ya kununua tiketi za Bahati Nasibu kwa urahisi kupitia mifumo ya kidijitali kama huduma za kifedha kwa njia ya simu, USSD codes, na Super App ya Mixx by Yas.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ITHUBA Tanzania, Kelvin Koka, ambaye ni mwendeshaji rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa kwa kipindi cha miaka minane, ushirikiano huu ni hatua muhimu katika kufanikisha uzinduzi huo:

“Bahati Nasibu ya Taifa Tanzania imeundwa kama rasilimali ya kitaifa inayolenga kutoa thamani, burudani, na manufaa ya kiuchumi kwa wananchi. Ushirikiano wetu na Mixx by Yas unadhihirisha dhamira yetu ya kushirikiana na taasisi zenye maono yanayolingana na yetu. Pamoja, tunaleta fursa jumuishi na rahisi kwa Watanzania wote,”

Kwa upande wake, Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Mixx by Yas, alielezea matumaini yao kuhusu ushirikiano huu: “Tunajivunia kuwa sehemu ya mpango huu wa mabadiliko. Bahati Nasibu ya Taifa ni fursa adhimu kwa Watanzania kushiriki kwa njia bunifu. Kupitia mifumo yetu ya kidijitali, tutahakikisha wateja wetu wanapata huduma hizi kwa njia rahisi na salama. Tunaamini ushirikiano huu utafungua milango mipya ya ubunifu na maendeleo,”

Ushirikiano huu unatarajiwa kubadilisha mfumo wa ushiriki wa Watanzania katika Bahati Nasibu ya Taifa kwa kuchanganya miundombinu madhubuti ya kidijitali ya Yas Tanzania na mikakati thabiti ya ushirikishwaji wa wateja. Kwa kuunganisha huduma hizi kupitia Super App ya Mixx by Yas, mamilioni ya Watanzania wataweza kununua tiketi, kupata maudhui maalum, promosheni, na taarifa za papo kwa papo kwa urahisi zaidi.

Kadri maandalizi ya uzinduzi rasmi yanavyoendelea, ushirikiano huu unaweka kiwango kipya cha ushirikiano wa kidijitali katika tasnia ya Bahati Nasibu nchini, huku ukitarajiwa kuongeza hamasa na ushiriki mpana wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.