top-news-1350×250-leaderboard-1

Bahati nasibu ya taifa yasaini mashirikiano na Vodacom kuwezesha miamala ya kidijitali

Na Mohammed Ulongo

Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania imesaını ushirikiano na jukwaa la huduma za kifedha kwa njia ya simu hapa nchini, Vodacom M-pesa, Ili kurahisisha miamala ya bahati nasibu ya Taifa na kupanua fursa za kibiashara kupitia mfumo wa fedha wa kidijitali

Akizungumza katika hafla fupi leo 27 Machi, 2025 Mkurugenzi wa ITHUBA Tanzania, Kelvin Koka amesema Kuunganishwa kwa bahati nasibu ya Taifa kwenye jukwaa la M-Pesa, kutawapa watumiaji urahisi wa upatikanaji wa michezo ya bahati nasibu kupitia jukwaa salama.

Pia, Koka amesema kutumia mtandao mpana wa Vodacom wenye zaidi ya watumiaji milioni 26, ushirikiano huu utawezesha urahisi wa ununuzi wa tiketi za michezo ya kubahatisha, kupitia majukwaa ya kidijitali ya Vodacom, ikiwemo huduma za M-pesa kwa njia ya simu.

Aidha, Kelvin Koka, ameelezea kuwa ushirikiano huwo ni hatua kubwa katika sekta ya michezo ya kubahatisha nchini na itasaidia kuwa na uwazi kwa washiriki wa jukwaa hilo. “Ushirikiano huu na M-Pesa utahakikisha kwamba wachezaji wanashiriki kikamilifu katika michezo ya bahati nasibu, huku ukihamasisha wafanyabishara kuweza kushirikiana kwa kuzingatia uwazi na mustakabali ujao wa bahati nasibu ya Taifa. Kwa kuwa M-Pesa ni mshirika rasmi wa huduma za kifedha na kunazingatia usalama, na uhakika wa miamala ya wateja wetu.”

Kwa upande wake Kelvin Nyanda, Kaimu Mkuu Idara ya M-PESA ambaye amemwakilisha Bi. Jacqueline Ikwabe, amesema, “M-Pesa imejikita katika kuwezesha uvumbuzi wa kidijitali unaowanufaisha wafanyabiashara na wateja Kwa kuiunganisha Bahati Nasibu ya Taifa kwenye jukwaa letu, tutahakikisha ushiriki salama, wa haraka na rahisi huku tukifungua fursa zaidi za ushirikiano katika sekta mbalimbali.” Amesema

Hata hivyo Nyanda amewatoa hofu watanzania juu ya wasiwasi wa uarifu wa kimtandao kwa miamala itakayofanyika nakusema Vodacom imejidhatiti kutumia fursa waliyoipata ya mashirikiano na Bahati Nasibu ya Taifa kwani nisehemu muhimu ya kuonesha ukubwa wao katika huduma.

Bahati nasibu ya Taifa inalenga kutumia ushirikiano huu kuongeza uelewa wa huduma zake na kuimarisha uaminifu kabla ya uzinduzi rasmi wa Bahati nasibu ya Taifa. Hatua hii inatarajiwa kuweka msingi wa ushirikiano katika sekta ya michezo ya kubahatisha na fedha nchini Tanzania

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.