Na Mohammed Ulongo
Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la kuombea Amani na Uchaguzi Mkuu wa oktoba 2025 amewataka wanasiasa kutotumia lugha zisizofaa katika majukwaa lengo likiwa ni kuepuka msuguano utakaoweza kusababisha vurugu kwa baadhi yao.
Hayo yamebainishwa leo Machi 24, 2025 na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama wakati akizungumza katika kikao na waandishi wa Habari kilicho kuwa na lengo la kuutaarifu umma juu ya Tamasha la kuombea na Uchaguzi mkuu litakalofanyika mikoa 26 kuanzia jijini dar es salaam.
Aidha, Msama ameongeza kwa kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia kuwezesha kufanikiwa kwa tamasha hilo kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza nguvu katika kupigania kuendelea kuwepo kwa tunu ya amani hapa nchini.
“Lengo ni kuweka umoja na ushirikiano watanzania kuombea uchaguzi kufanyika kwa Amani na kupata viongozi ambao watatuongoza kwa hekima na busara hivyo ni wakati kwa wadau kujitokeza kusaidia kuwezesha tamasha hili ili kudumisha amani nchini”. amesema
Pia amesema, “Waimbaji kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda wanatarajia kupamba tamasha hilo la uimbaji na Maombi ya uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tamasha la Kuombea uchaguzi litafanyika hivi karibuni na lengo kuu ni kuwaunganisha waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili Ndani na Nje ya Tanzania.
Crédito: Link de origem