top-news-1350×250-leaderboard-1

Wananchi jitokezeni kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura

Na Mwandishi Wetu

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimehamasisha wanachama wake kujitokeza kwa wingi kwenye shughuli ya kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura ili kitete nafasi ya kushika dola.

Shughuli ya uboreshaji taarifa za mpiga kura zitakazo mwenzesha kila mtanzania kupata kibali cha kutumia haki yake ya kumchagua kiongozi anayemtaka inasimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na kwa mkoa wa Dar es Salaam linatarajiwa kuanza Machi 17 hadi 23 Mwaka huu.

Akihamasisha shughuli hiyo kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Wilaya ya Ubungo, ukiwakutanisha viongozi wa Chama hicho, Jumuiya ngazi ya Shina, tawi, mitaa, Kata na Wilaya, Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla amesema ili watete dola ni lazima wafuasi wao wajiandikishe kabla ya kuanza kuwashawishi watanzania wengine.

“CCM tunawachama 12 milioni nchi nzima lakini Dar es Salaam tunaongoza kwa idadi ya wapiga kura wengi ikilinganishwa na mikoa mingine, tusilale mtihani tulionao kwanza kuhakikisha idadi hiyo wanajitokeza kujiandikisha viongozi wa Wilaya, Kata, Matawi , Mitaa hadi Shina hakikisheni watu wenu wanaenda kujiandikisha, ” amesema Makalla .

Makalla mesema licha ya kuhitaji kutetea dola lakini uchaguzi ni namba kwani anayepata kura nyingi anatangazwa mshindi hivyo wasipuuze mchakato huo kama wanataka kuitawala nchi.

“Wapiga kura wako ngazi ya chini huku wilayani ni kuratibu tu lakini watu wako kwenye mashina, tawi na Kata kwahiyo watu wa wilayani tokeni simamieni kazi hiyo mkoani na mabalozi nayie wapeni ushirikiano tusifanye makosa,” amesema

Makalla ambaye ni mlezi wa mkoa wa Dar es Salaam kupitia chama hicho amesema hataki kuona wananchi wakimuangusha kupitia shughuli ya uboreshaji daftari la mpiga kura kwani walishafanya makubwa na hapaswi kujikwaa kwa jambo hilo.

“Mkitoka hapa wekeni kwenye ratiba zetu kuanzia Machi 17 hadi 23, 2025 na nyie kama viongozi anzeni na watu wenu wanaowazunguka na baada ya hapo anzeni kuhamasisha wengine ili tujihakikishie kura katika uchaguzi mkuu,” amesema.

Amesema wakati wakiendelea na majukumu hayo, viongozi wa serikali za mitaa waliochaguliwa wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuhakikisha ofisi zao zinakuwa kimbilio.

“Tunahitaji kuona wananchi wanapata huduma nzuri ili wafurahie hawakufanya makosa kumchaguzi kiongozi wa Chama cha mapinduzi,” amesema

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.