top-news-1350×250-leaderboard-1

Rais Samia afanya uteuzi, yumo mrithi wa Profesa Janabi

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ikiwemo Dk Delilah Kimambo kuwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Dk Kimambo anachukua nafasi Profesa Mohammed Janabi ambaye alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.

Profesa Janabi ambaye alikula  kiapo cha kushika nafadi hiyo Mei 28, 2025 ikiwa zimepita siku 11 tangu alipochaguliwa Mei 18, 2025.

Alichaguliwa wakati wa kikao maalumu cha ana kwa ana cha kamati ya kanda ya WHO ya Afrika na bodi hiyo ya utendaji kilichofany1ka Geneva, Uswisi hivyo kuacha nafasi aliyokuwa akiishikilia awali ya kuwa kiongozi mkuu wa MNH wazi.

Dk Delilah ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 16, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka awali alikuwa akifanya kazi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Mbali naye pia Rais Samia amemteua Jaji mstaafu Hamisa Hamis Kalombola kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha pili.

Pia kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Sharifa Nyanga, Paul Thomas Sangawe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa SELF kwa kipindi cha pili.

“Pia Jaji Rose Ally Ebrahim ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza Ushindani (Fair Competition Tribunal) huku Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia,” imeeleza taarifa hiyo.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.