top-news-1350×250-leaderboard-1

Matukio ya ubakaji, ulawiti yapungua nchini

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amesema wizara yake imeshughulikia migogoro ya ndoa 97,234 katika kipindi cha Julai hadi kufikia Aprili 2025 kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii ngazi ya halmashauri hadi taifa.

Dk Gwajima ametoa takwimu hizo leo Jumanne Mei 27, 2025, bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Pia amesema mashauri 81, 820 yalipatiwa ufumbuzi 15,414 yalipelekwa mahakamani kwa hatua zaidi huku wizara hiyo kwa kushirikiana na wizara za kisekta na wadau imeendelea kuratibu huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi dhidi ya watoto.

“atika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025, manusura 19,717 waliripotiwa wakiwemo watoto 7,278, wa kiume 1,373 na wa kike 5,905 na watu wazima 12,439 ambao wote walipata huduma katika madawati ya jinsia na watoto ya polisi nchini ambapo pia maofisa ustawi wa jamii huwa wapo,” amesema Dk Gwajima.

Dk Gwajima amesema vitendo vya ubakaji vimepungua kutoka matukio 8,185 mwaka 2023 hadi 7,670 sawa na kupungua kwa asilimia 6.3, huku matukio ya ulawiti yakipungua kutoka matukio 2,382 mwaka 2023 hadi 1.930 sawa na kupungua kwa asilimia 9 mwaka 2024.


Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.