Dar es Salaam. Wataalamu wanasema kuna baadhi ya faida za kiafya zinazopatikana kwa kunusa harufu ya ushuzi.
Ushuzi hujumuisha asilimia 59 ya gesi ya naitrojeni, asilimia 21 ya haidrojen, asilimia tisa ya hewa ukaa, asilimia saba ya methane na asilimia nne ya oksijeni.
Kila binadamu hutoa ushuzi kulingana na wingi wa gesi tumboni, hata ukiubana lazima ukutoke uwapo usingizini.
Inaelezwa kuwa ushuzi wa kimya una afya zaidi kuliko ule unaoambatana na sauti mbalimbali, na kwamba ukiona hali hiyo nenda ukatibiwe.
Hata hivyo, kuwa na gesi nyingi au gesi inayotokea na dalili nyingine inaweza kuashiria hali ya kiafya inayohitaji uchunguzi zaidi.
Mtaalamu wa afya ya jamii, Dk Paul Masua anasema kutoa ushuzi ni kutoa kitu ambacho hakihitajiki mwilini, ni uchafu unaotoka au hali fulani ya mwili katika kupumua kuondoa vitu ambavyo havihitajiki, akisema hewa inayotoka inasaidia hata kwenye tumbo ili nako kupumue, kwani tumbo lazima liwe na gesi.
“Gesi hii inatoka wapi? Inatokana na jinsi chakula kinavyomeng’enywa tumboni, ndiyo maana inategemea umekula chakula gani. Kingine hakitoi ushuzi, lakini kingine ukikila kinatoa ushuzi mkali,”anasema na kuongeza:
“Kwa mfano, mtu anapokula mayai, ile salfa kutoa harufu kali ni upumuaji. Ni hali fulani ya mmeng’enyo wa mwili, na ndiyo maana kama kukiwa na gesi imezidi sana mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula nao unakuwa na shida na kwahiyo utahitajika kumuona daktari.’’
Kwa mujibu wa mtandao wa Apollo247, watafiti wamegundua manufaa ya kunusa ushuzi wako mwenyewe, ikiwamo kuboresha utendakazi wa mitokondria (sehemu ya seli zako inayosaidia kuzalisha nishati) mwilini, jambo ambalo pia husaidia kupunguza hatari ya magonjwa sugu.
Kwa kawaida, gesi ya tumboni ni jambo la kawaida kabisa. Lakini vipi kuhusu ile gesi yenye harufu mbaya sana, inawezekana kuwa na manufaa kiafya?
Hebu fikiria: Uko na mtu unayemheshimu sana. Kisha, ghafla unaisikia. Labda ni kama mshindo mkubwa au labda ni mluzi wa kimya.
Ingawa hisia yako ya kwanza ni kukimbia hadi chumba kingine kujinusuru na harufu, unaweza kutaka kufikiria upya.
Utafiti wa hivi karibuni kwa wanyama unaonyesha kuwa hidrojeni salfaidi, gesi inayotoa harufu kama ile ya ‘yai bovu’ kwenye gesi ya kinyesi, inaweza kuwa na faida fulani kwa afya ya binadamu.
Faida hizo zinaweza kujumuisha kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, figo na hata kusaidia ubongo.
Utafiti uliofanywa mwaka 2014 na timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Exeter kilichopo Uingereza na Chuo Kikuu cha Texas, unaeleza kwamba kunusa hidrojeni salfaidi, kunaweza kuwa jambo zuri kwa afya yako.
Utafiti huu uliegemea wazo kwamba mitochondria, yaani sehemu ya seli zako inayosaidia kuzalisha nishati, inaweza kufaidika na gesi hii.
Katika utafiti huu, watafiti waligundua kwamba wakati seli kwenye mishipa ya damu au mshipa wa damu zinapopatwa na uharibifu au shinikizo linalohusiana na hali fulani, seli hizi hutumia vichocheo (enzymes) vya mwili kuzalisha hidrojeni salfaidi.
Gesi hii kisha inaruhusu seli kudhibiti vyema shinikizo la oksidi linalohusiana na hali hizi, ambalo mwishowe linasababisha uvimbe ambao unaweza kuua seli.
Lakini hali inapokuwa mbaya zaidi, mitochondria haziwezi kuzalisha gesi hii kwa wingi wa kutosha ili kuendelea kusaidia na ugonjwa unaendelea kuwa mbaya zaidi.
Watafiti walijaribu nadharia moja; je, kuziweka seli kwenye hidrojeni salfaidi ya bandia kunaweza kusaidia kuweka mitochondria imara na kuzuia magonjwa kuwa mabaya zaidi?
Kwa hiyo, walitengeneza kiwanja kilichoitwa AP39 ambacho kilifanya kazi kama hidrojeni salfaidi. Kisha walikifanya kiwanja hiki kiwepo kwenye seli kwenye mishipa ya damu.
Matokeo ya awali yanaonyesha kwamba hadi asilimia 80 ya mitochondria zilizowekwa kwenye AP39 zililindwa na gesi hii. Hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa hali nyingi zinazohusiana na kifo cha seli kinachohusiana na utendaji wa mitochondria.
Utafiti zaidi unahitajika kuhusu mwingiliano wa AP39/hidrojeni salfaidi na mifumo mingine ya mwili, lakini matokeo ya awali ni ya matumaini.
Matokeo haya hayakuwa bahati tu. Mwaka huo huo, timu yenye baadhi ya watafiti haohao iligundua kwamba AP39 ililinda mitochondria kutokana na uharibifu ulioletwa na uvimbe.
Yaliyobainika utafiti wa AP39
Utafiti wa awali kuhusu AP39 ulifanyika kwa wanyama pekee na kubaini mambo ambayo kiwanja hicho kinaweza kufanya kwa binadamu.
Mosi, kupunguza shinikizo la damu. Utafiti wa mwaka 2015 uligundua kwamba AP39 inaweza kufanya kuta za mishipa ya damu kuwa laini zaidi, hivyo kupunguza shinikizo la damu.
Pili, kutibu shambulio la moyo na kiharusi. Utafiti wa 2018 unapendekeza kwamba AP39 inaweza kupanua mishipa ya damu na kufanya ionekane ikituma damu kwa ufanisi zaidi, mwishowe hali hiyo inaweza kutibu shambulio la moyo au kupunguza hatari ya kiharusi.
Tatu, kuboresha afya ya figo. Utafiti wa 2016 unapendekeza kwamba AP39 inaweza kutibu figo zilizoathiriwa na uvimbe.
Kulinda ubongo wako. Utafiti wa 2015 unapendekeza kwamba AP39 inaweza kulinda ubongo kutokana na uharibifu baada ya shambulio la moyo. Utafiti wa 2016 unapendekeza inaweza kuzuia dementia au magonjwa mengine ya kukosa kumbukumbu.
Nne, kupunguza madhara ya kuzeeka. Utafiti wa 2018 unapendekeza kwamba AP39 inaweza kulinda miundo ya seli inayodhoofika kwa muda.
Wazo kuu linaloongoza katika tafiti hizi zote ni kwamba hidrojeni salfaidi inapunguza madhara ya shinikizo la oksidi kwenye seli. Hii inasaidia seli kuendelea kuwa imara na kudumu kwa muda mrefu zaidi.
Kama ilivyo kwa gesi nyingi, hata gesi yenye ushuzi, ni ya kawaida kabisa. Lakini kuwa na gesi nyingi au gesi inayotoa ushuzi mkali sana kunaweza kumaanisha kwamba kuna shida ya kiafya inayohitaji uchunguzi.
Kwa mujibu wa mtandao wa health.clevelandclinic, wanashauri kumuona daktari ikiwa una dalili zifuatazo pamoja na gesi nyingi au gesi yenye ushuzi mkali kuliko kawaida.
Muone daktari ikiwa unapata maumivu makali, kujisikia kuziba tumbo, kujisikia mgonjwa, kutapika, kukosa choo, kuharisha na kupoteza uzito kwa kawaida.
Ushuzi unaweza kuwa mzuri kwa kunusa mara kwa mara, hata hivyo kuna vidokezo vya kupunguza gesi na kuziba tumbo ikiwa gesi yako inahusishwa na matatizo ya tumbo.
Kula polepole. Unapokula kwa haraka, unameza hewa zaidi ambayo inaweza kuwa gesi katika utumbo wako. Kula taratibu ili kupunguza hewa unayomeza.
Kunywa maji mengi. Kukosa choo kunaweza kusababisha haja kubwa kubaki kwa muda mrefu tumboni.
Hii inaweza kusababisha maumivu ya tumbo na kuzalisha gesi yenye ushuzi mkali kuliko kawaida. Maji husaidia kupunguza haja kubwa na kuhakikisha matokeo ya haja kubwa kuwa ya kawaida.
Epuka vinywaji vyenye kaboni. Soda, bia na vinywaji vyenye kujaa kaboni vyote vina hewa, ambayo inaweza kuwa gesi katika utumbo wako.
Punguza kidogo vyakula vya nyuzinyuzi kama matunda, na maharage, kwani vyote vinaweza kuleta gesi nyingi.
Crédito: Link de origem