mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
wote wanatakiwa kufika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo
Chogo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi
tarehe 18 Mei, 2025 bila kukosa; kwa ambaye hatafika chuoni kwa tarehe
zilizopangwa hatapokelewa na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.
Kufika
chuoni shuka kituo cha Kabuku kilichopo kilometa 12 toka chuoni. Chuo
kimeandaa utaratibu maalumu wa kuwapokea kwa tarehe zilizotajwa hapo
juu, kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku.
Mhusika atapaswa kujigharamia nauli ya kwenda sambamba na chakula na malazi kwa siku zote ambazo atakuwa hajapokelewa Chuoni.
Mhusika
anapaswa kuja akiwa na vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi
alioombea pamoja na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha NIDA au namba
na leseni hai kwa walioomba nafasi ya udereva. Vyeti vyote tajwa hapo
juu viwe na nakala tatu kwa kila cheti pia vyeti hivyo vitakaguliwa na
kwa ambaye majina yake yatatofautiana kati ya vyeti vya shule/taaluma,
NIDA na cheti cha kuzaliwa watarudishwa na nafasi zao zitachukuliwa na
wengine.
Mhusika atakapofika chuoni awe tayari kupimwa afya ya
mwili, akili na Mimba kwa wanawake na ambaye atabainika kuwa na kasoro
za kiafyahataruhusiwa kuendelea na mafunzo na atarudishwa kwa gharama
zake na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.
Wahusika wote
wanatakiwa kuja na vifaa vifuatavyo: mashuka mawili (02) ya rangi ya
bluu, mto 01 na foronya 02 ya rangi ya bluu, chandarua 01 rangi ya bluu
(cha duara), ndoo ya plastiki ya lita 20, sahani na kikombe cha bati,
fedha kiasi kwa matumizi binafsi na bima za afya kwa walionazo. Aidha
vifaa vifuatavyo watanunua kwenye duka la Chuo, raba za michezo, fulana
(T-shirt) rangi ya bluu, Madaftari makubwa (counter books 4 quire 5
pcs), vifaa vya michezo (truck suite, bukta bluu, na fulana) na kalamu.
Crédito: Link de origem