top-news-1350×250-leaderboard-1

CCM yatoa ratiba kwa wanaotaka ubunge, udiwani, uwakilishi

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetanganza kufungua dirisha kwa wanachama wake wanaotaka kuwania udiwani, uwakilisha na ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Chama hicho tawala nchini Tanzania kimesema fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hizo zitaanza kutolewa Mei 1-15, 2025.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Alhamisi, Aprili 10, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla imeelezea utaratibu kuwa wanachama wanaogombea nafasi ya ubunge au ujumbe wa Baraza la Wawakilishi watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika.

Makalla amesema wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi, kupitia kundi la Umoja wa Wanawake (UWT) pamoja na makundi maalumu NGO, wafanyakazi, wasomi na wenye ulemavu watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa UWT wa Mkoa unaohusika.

Amesema wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitia jumuiya ya Vijana wa chama hicho (UVCCM) watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa UVCCM Mkoa unaohusika.

Makalla amesema wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitia jumuiya ya wazazi watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa Wazazi Mkoa unaohusika.

Amesema Wanachama wanaogombea nafasi ya Diwani wa Kata (Bara) au Wadi (Zanzibar) watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Kata/Wadi inayohusika.

Amesema wanachama wanaogombea nafasi ya Udiwani Viti Maalumu vya Wanawake watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa UWT wa Wilaya inayohusika.

Katika nafasi ya urais, chama hicho kilikwisha kumaliza kwa kumteua Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza. Upande wa Zanzibar, Rais Hussein Mwinyi alipitishwa kutetea nafasi hiyo.

Crédito: Link de origem

Leave A Reply

Your email address will not be published.