top-news-1350×250-leaderboard-1

Zahanati yenye mtumishi mmoja, anayetoa huduma vijiji vitatu

-Wananchi waelezamadharayaliyowapata

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Agosti 18, mwaka 2023 ni siku ambayo, John Chalya,mkazi wa kijiji cha Mwamanenge wilaya ya Maswa mkoani Simiyu hatoisahau katika maisha yake, kutokana na kumpoteza mtoto wake, Nkamba John (3) ambaye alifariki dunia kwa kukosa huduma katika zahanati ya kijiji hicho ambayo inamhudumu mmoja tu.

Chalya anasema siku hiyo majira ya saa 3:20 usiku akiwa nyumbani kwake na familia yake yenye mke nawatotowa nnewakijiandaakulala mara baada ya kukupata mlo wa usiku, mke wake, Hollo Jidayi alimjulisha mtoto wao mdogo alikuwa na joto kali.

John Chalya,mkazi wa kijiji cha Mwamanenge.

Anasema kadri muda ulivyokuwa ukienda hali ya mtoto huyo ilizidi kubadilika kwa maana ya joto kuzidi kupanda, hivyo alishauriana na mke wake wampeleke mtoto huyo katika zahanati iliyopo katika kijiji hicho ili aweze kupatiwa  matibabu.

Anasimulia  kuwa alimchukua mtoto wake huyo na kumbeba mgongoni, kisha kutumia usafiri wa baiskeli kwenda hospitali, lakini alipofika katika zahanati hiyo alikosa huduma.

Chalya anasema zahanati hiyo ya kijiji cha Mwamanenge ili kuwa imefungwa kwa kile kilichoelezwa kwamba muuguzi pekee anayetoa huduma hakuwepo wakati huo.

“Nilipofika katika zahanati ya kijiji chetu ilikuwa imefungwa na nilipomuuliza mlinzi kuwa nesi yuko wapi ambaye ndiye mhudumu pekee katika zahanati hiyo nikaambiwa kuwa hayupo,” alisema Chalya.

Anasema katika kujaribu kuokoa maisha ya mtoto wake, ilimlazimu kumkimbiza katika kituo cha afya cha Zebeya umbali wakilomita 20 lakini mtoto wake alifariaki akiwa njiani kabla ya kufika.

“Mimi nilishapoteza mtoto wangu, nilifika katika zahanati hii nyakati za usiku baada ya mwanangu kushikwa na homa kali sikupata huduma kabisa kutokana na mhudumu huyu kutokuwepo ikanilazimu nilisafiri naye kwenda kituo cha afya cha Zebeya tukiwa njiani halii kabadilika ikawa mbaya akafariki,” alisema.

Chalya alikuwa akizungumza na Mwandishi wa habari wa makala hii kuhusu adha ambao wakazi wa Kijiji cha Mwamanenge na vijiji vingine jirani wanaopata kutokana na zahanati ya  Kijiji hicho kuwa na muhudumu mmoja.

Nini kinachosababisha kadhia hiyo?

Kadhia hiyo inasababishwa na kuwepo kwa mtumishi mmoja katika zahanati hiyo ambaye ni muuguzi anatoa huduma kwa vijiji vitatu vinavyotegemea kupata matibabu katika zahanati ya Mwamanenge.

Huduma ambazo amekuwa akitoa ni pamoja na kutoa huduma za kitabibu, famasi ana maabara ambazo si majukumu yake hivyo amekuwa akitumia uzoefu tu kwa zile huduma ambazo anaweza kuzimudu kwa kiwango kidogo ili kuwasaidia wananchi wa eneo hilo.

Vijiji vinavyopata huduma kwenye zahanati hiyo ni pamoja na Mwamanenge, Iwelimo na Mwangholo vyenye wakazi zaidi ya 12,000.

Licha ya mwongozo wa utumishi wa mwaka 2014 kuagiza kuwa kila zahanati iwe na watumishi wasiozipungua 10, hali ni tofauti katika zahanati hiyo nakusababisha kuzorota kwa utoaji wa huduma za afya.

Hata hivyo wakati mwingine zahanati hiyo imekuwa ikisitisha kutoa hudum akwa kile kilichoelezwa kuwa Muuguzi huyo ambaye ndiye Mfawidhi wa Zahanati, kuwa kwenye majukumu mengine ya kikazi.

Mashuhuda wengine wasimulia

Miongoni mwa mashuhuda ambao ni waathirika wa uhaba wa wahudumu wa afya katika zahanati hiyo ,ni Mama Mjamzito, Rahel Seme mkazi wa kijiji cha Iwelimo ambaye anasema kuwa kuna wakati wanalazimika kushinda njaa kutwa nzima na hurudi nyumban ibila kuhudumiwa kutokana na wingi wa wagonjwa.

“Nimefika hapa tangu asubuhi, huduma hii ni kama mnavyoiona mhudumu yuko mmoja anahudumia huko anarudi kule, akitoka kule anakwenda kule yaani hakuna huduma.”

“Siku nyingine tunakuja tarehe za kliniki zilishafika anaona watu wengi muuguzi anatuambia rudini mje kesho nishaelemewa na ukiangalia ni kwelii nabidi tuondoke tu,” alisema.

Mkazi mwingine wa kijij ihicho, Victoria James alisema kuwa zahanati kutokana n au chache wa watumishi wananchi wanalazimika kuwa wa pole kwa kila jambo wanaloelezwa hata kama hawakubaliani nalo.

“Zahanatii inahudumia vijiji vitatu na wahudumu hawatoshi mmoja anaweza kufanyakazi kutwa nzima, hata akigoma hatuwezi kumuonya kwa sababu ana kuwa na uchovu,” alisema.

Walwa Jidai mkazi wa kijiji cha Iwelimo alisema kuwa wamekuwa wakiahidiwa na viongozi wa siasa wakati wa kampeni za uchaguzi, lakini wakichaguliwa hawatekelezi.

 “Kila unapofika uchaguzi, wanasiasa wanakuja hapa kutuomba kura na kuahidi kuongeza wahudumu katika zahanati yetu, lakini uchaguzi ukiisha wanatutelekeza na wala hawakumbuki ahadi zao,” alisema.

Kauli ya Muuguzi

Muuguzi wa zahanati hiyo, Kwiligwa Shija alisema uhaba wa wahudumu unaleta changamoto ya kuhudumia wakazi hao wapatao 12,000 katika vijiji hivyo vinavyotegemea huduma ya zahanati ya Mwamanenge.

“Niko pekee yangu mtumishi katika zahanati hii ni mzigo mzito kuwa hudumia     watu wote hao, hata hivyo napambana hivyo hivyo,” alisema.

Alisema kuwa anafanya kazi katika mazinigira magumu sana kwani shughuli zote za tiba zikiwemo za ukunga pamoja na utawala anazifanya mwenyewe na hivyo tija yake ina kuwa ni ndogo.

“Ukiangalia mimi napaswa kufanyakazi ya Afya ya Mama lakini kwa hali iliyopo nafanyakazi zote zikiwemo za utabibu, ukunga, ugawe dawa, maabara na utawala hapa huwezi kujigawa kwa mtu mmoja na wala huwezi kutimiza majukumu haya kwa tija,” alisema.

Wasemavyo viongozi wa kisiasa

Akizungumzia kadhia wanayopata wagonjwa, Diwani wa Kata ya Mwamanenge, Petro Mwandu alisema zahanatihiyo inakabiliwa na uhabawawatumishi kwamuda mrefu na walishachukuahatua lakini hakuna utekelezaji.

“Kama mwakilishi  wa wananchi wa Kata hii nilishafikisha suala hili katika vikao mbalimbali vya halmashauri ya wilaya likiwemo baraza la madiwani na kupatiwa ahadi ya kupatiwa wa hudumu wengine akiwemo mganga lakini hadi sasa ni miaka miwili hakuna utekelezaji wowote,” alisema.

Mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo.

Mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo alisema kuwa licha yakuwepo kwa upungufu wa wahudumu katika zahanati hiyo lakini huduma za afya zimekuwa zikitolewa kwenye kijiji hicho na kata kwa ujumla.

Alisema kuwa wamekuwa wakipiga kelele bungeni kwa serikali ili iweze kutoa kibali cha kuajili watumishi wa kada ya afya na zimekuwa zikitolewa lakini ni chache  kutokana na uwezo wa serikali kuwa mdogo licha yamahitaji kuwa makubwa.

Mkurugenzi halmashauri azungumza

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Maswa ,Maisha Mtipa amekiri kuwepo kwa changamoto hizo  za upungufu wa watumishi katika sekta ya afya huku zahanati nyingine zikishindw akufunguliwa kutokana na kuwepo kwa uhaba wa watumishi.

 “Tunajua wananchi wetu wanapata  changamoto ya kupatiwa huduma  za afya zipasavyo kwenye maeneo yenye upungufu wa watumishi wa kada ya afya,na zipo zahanati tumeshindwa kuzifungua licha ya majengo kukamilika,kwa umuhimu wa zahanati ya Mwamanenge tutapeleka watumishi wawili akiwemo mganga na muuguzi mmoja ili waweze kumsaidia mtumishi mmoja aliyepo kwa sasa,”alisema..

Naibu Waziri wa Afya

Alipoulizwa kuhusu kadhia hiyo kwa njia ya simu, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amekiri kuwepo kwa upungufu wa watumishi wa sekta ya afya, akisema mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa tisa yenye upungufu mkubwa zaidi.

“Tumechukua hatua kadhaa ikiwemo kuajiri watumishi wa kada ya afya katika kipindi hiki cha bajeti ya mwaka 2024/2025 mikoa na halmashauri ambazo zina upungufu ikiwemo wilaya ya Maswa wamepelekwa.”

 “Sambamba na ajira mpya tumezielekeza mamlaka za mikoa (Katibu tawala wa mkoa) na halmashauri kuwatanya watumishi wa afya ndani ya maeneo yao ilikuweka uwiano mzuri,” anasema.

Sera ya Afya ya mwaka 2007 inaelekeza kila kijiji kuwa na zahanati na kila kata kuwa na kituo cha afya vyenye watumishi wa kutosha.

Crédito: Link de origem

Comments are closed.